Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema haki, demokrasia, sheria na utawala bora utadumishwa kwa watu wote wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa 2024.

Rais Samia amesema hayo katika sherehe za mwaka mpya 2024 (Diplomatic Sherry Party) kwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapq nchini pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa zilizofanyika Ikulu.

 

Amesema, ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, Kikosi Kazi huru cha kupitia na kushauri mageuzi muhimu katika mfumo wa siasa kiliundwa ambapo kiliwasilisha ripoti yake mwaka 2023.

Rais Samia pia amesema mapendekezo mengi ya Kikosi Kazi yaliyopokelewa na serikali na wadau wote yalihusu kuongeza uwazi katika michakato ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.

Ameongeza kuwa, masuala machache hayakupokelewa moja kwa moja ambayo yalikuwa kinyume na katiba hivyo yanaweza kuchukuliwa wakati wa mchakato wa marekebisho ya katiba.

Rais Samia pis amesema serikali itaendeleza ushirikiano na balozi hizo kwa mujibu wa katiba, tunu za kitaifa, usawa, umoja na mshikamano wa kitaifa huku akiwataka mabalozi hao kutokuingilia uchaguzi na kuzingatia mila, kanuni na maadili ya kidiplomasia.

Makundi maalum yapewe kipaumbele ununuzi wa Umma - Dkt. Biteko
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 8, 2024