Takribani abiria 51 wamenusurika kifo, baada ya basi la Umma Express walilokuwa wakisafiria kusombwa na mafuriko katika barabara kuu ya Garissa-Nairobi.

Ajali hiyo iliyotokea Aprili 8, 2024, ilizusha taharuki na kupelekea juhudi za ziada ili kuwaokoa Abiria hao waliokuwa safarini kuelekea jijini Nairobi ambapo wote waliokolewa salama katika eneo la Areri.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kaunti ya Tana River, All Ndiema amesema watu 51 waliokuwa kwenye basi hilo wakisafiri kutoka Garissa kuelekea Nairobi majira ya saa 11:30 jioni basi hilo liliposombwa na mafuriko eneo la Lager Areli.

Majaliwa: Tuendelee kuuenzi, kuulinda Muungano wetu
Aziz Ki afunguka alichoongea na Mokwena