Viongozi wa dini mkoani Manyara, wameombwa kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia, ikiwemo vya ubakaji ambavyo vimekithiri Mkoani humo.

Wito huo, umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara SACP, George Katabazi wakati harambee ya kukusanya shilingi milioni 100 za upanuzi wa eneo la Msikiti Mkuu wa Mkoa wa Manyara Masjid Rahma wa mjini Babati.

Naye Sheik wa Mkoa wa Manyara, Mohamed Kadili kwa niaba ya Viongozi wa dini ameahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi kukemea maovu mkoani humo.

Aidha, katika Harambee hiyo zaidi ya shilingi millioni 2 zimechangwa ambapo Kamanda Katabazi amechangia shilingi 600,000.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 20, 2024
Majaliwa ataka maonesho ya Nishati yaboreshwe