Rapa Izzo Bizness, anayetamba na wimbo wa ‘Umeniweza’ ameweka wazi kwamba dawa za kulevya ndizo zilizoshusha viwango vya baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini.
Izzo alidai hataki kuingia ndani zaidi katika masuala hayo, lakini anaamini wasanii wengi wa muziki huo wameshuka viwango vyao vya kuimba na kutunga kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
”Kwa upande wangu sina mengi ya kusema kuhusu matumizi haya ya dawa za kulevya kwa wasanii, ila nawaasa nguvu kazi za vijana na kuondoa thamani ya utu wao kwa jamii ni bora waachane nazo kwa faida yao na nchi kwa ujumla,” amesema Izzo biznes.
Izzo alizungumza hayo kutokatana na idadi kubwa ya wasanii kuhusishwa katika sakata la madawa ya kulevya huku wakiwa hawafanyi vizuri katika sanaa ya muziki katika utungaji na uimbaji.
Msemo wa Izzo bizness unadhihirishwa moja kwa moja kwa kuangalia idadi kubwa ya wasanii waliopo kwenye sanaa kwa sasa wengi wao ni wasanii chipukizi, wakongwe wa muziki wengi wao wametokomea kusikojulikana wakati wengine wakiwa wamejihusha moja kwa moja na usambazaji, utumiaji wa madawa ya kulevya kitu ambacho ni hatarishi kwa afya zao na taifa kiujumla.