Chama cha ACT- Wazalendo kitafanya uzinduzi wa kampeni zake leo katika viwanja vya Zakheim, jijini Dar es Salaam.

Chama hicho kitatatambulisha ilani yake ya uchaguzi ambayo inatajwa kuwa tofauti kabisa na ilani za vyama vingine kutokana na mtazamo wa sera za kijamaa zinazotumiwa na chama hicho.

Aidha chama hicho kitaanza kumpigia kampeni rasmi mgombea urais wake, Bi. Anna Mghira ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho, pamoja na wagombea ubunge na udiwani katika majimbo mbalimbali nchini.

Katibu wa mipango na maendeleo na Mikakati wa ACT-Wazalendo, Habibu Mchange alisema kuwa maandalizi ya hafla hiyo yamekamilika na kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kusikiliza sera za chama hicho.

“Tunawakaribisha wananchi waje kusikiliza kampeni za kisayansi. Na ndio maana tumeamua kuwaita wagombea wote wa ubunge kuhudhuria na kuwatambulisha kwa wananchi,” alisema Habibu Mchange.

Kampeni hizo zitaongozwa na kiongozi mkuu wa chama hicho aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Zitto Kabwe.

 

Sitta Amvaa Lowassa Ufisadi, Ataka Mdahalo Naye Wiki Hii
“Lowassa Ametuangusha Kwenye Uzinduzi”