Katika tukio la kusitikisha, Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma, Emmanuel Meta mwenye umri wa miaka 37 ameuawa kikatili kwa kupigwa mapanga na watu wasiojulikana.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), David Mnyambuga, alieleza kuwa afisa huyo alivamiwa na kukatwa na mapanga Januari 20 mwaka huu majira ya saa 6:15 usiku. Alisema kuwa Meta alifariki wakati akipatiwa matibabu kufuatia kipigo hicho.

Kaimu Kamanda huyo alieleza kuwa Jeshi la polisi linamshikilia mtu mmoja kufuatia tukio hilo kwa ajili ya mahojiano.

 

Mganda Asajiliwa Ubelgiji Badala Ya Mbwana Samatta
Kranevitter Azigonganisha Chalsea Na Arsenal Mjini Madrid