Edward Lowassa, mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ameendelea kuzihesabu siku za zilizobaki kabla ya Uchaguzi Mkuu, Octoba 25 huku akiwahimiza wananchi kufanya maamuzi sahihi.

Mgombea huyo ambaye alifanya mkutano mkubwa jana katika jimbo la Kawe aliwakumbusha wananchi hao kuwa zimebaki siku 48 za kuamua kama wamataka kuendelea na maisha ya shida au kufanya mabadiliko katika kuleta maendeleo huku akishangiliwa na umati uliohudhuria.

“Zimebaki siku 48 kukubali ajira ya vijana kwa wingi katika taifa letu, zimebaki siku 48 tukatae tatizo la maji hapa Dar es Salaam, zimebaki siku 48 tukatae adha wanayopata watu katika vituo vya afya, zimebaki siku 48 tukatae michango ya shule za sekondari na shule za msingi,” alisema Lowassa ambaye amekuwa akihesabu siku jukwaani kila anapokuwa.

Katika hatua nyingine, Lowassa aliahidi kuondoa tatizo la foleni katika jiji la Dar es Salaam, ahadi ambayo ilitiliwa msisitizo na mgombea mwenza, Haji Duni Haji aliyewaambia wananchi mkoani Tanga kuwa serikali yao itahakikisha inaleta treni za umeme katika jiji la Dar es Salaam.

Hiyo ni ahadi mpya toka kwa wagombea hao wanaoongozwa na kauli mbiu ya ‘mabadiliko’.

Idadi ya Waliofariki Kwenye Mkutano Wa Magufuli Yaongezeka
Venus Williams Atamba Kumaliza Uteja Kwa Serena