Mabingwa wa Soka nchini Sudan Al Merrikh wamewasili mjini Kinshasa, DR Congo tayari kwa mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya Makundi dhidi ya AS Vita Club.

Wawili hao ambao tayari wameshatupwa nje ya michuano hiyo, watapapatuana Ijumaa (April 09), kwenye uwanja wa Martyrs (Stade des Martyrs), huku AS Vita Club wakihitaji heshima ya kushinda nyumbani.

Al Merrikh wameamua kuelekea mapema mjini Kinshasa, DR Congo ili kuweka kambi kwa siku kadhaa kabla ya mchezo, hatua ambayo imeonesha wamedhamiria kupambana na kupata matokeo mazuri ugenini.

Hata hivyo viongozi wa klabu hiyo hawajazungumza lolote tangu alipowasili mjini humo, lakini kuwasili kwao mapema kunadhihirisha wamejizatiti kufanya vizuri dhidi ya AS Vita Club.

Mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo mjini Khartoum, Sudan mwezi Machi,  Al Merrikh walifungwa mabao manne kwa moja, jambo ambalo linachukuliwa kama chagizo kwao la kulipa kisasi.

AS Vita Cub wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ‘Kundi A’ kwa kufiksha alama 04, Al Merrikh wanaburuza mkia wa kundi hilo kwa umiliki alama 02, huku Simba SC wakiongoza msimamo wa kundi hilo kwa kufikisha alama 13 na Al Ahly wapo nafasi ya pili kwa kuwa na alama 08.

Rais Samia aagiza vyombo vya habari vilivyofungwa vifunguliwe
Simba SC kuifuata Al Ahly