Algeria imetangaza kikosi cha awali cha wachezaji 33 kwa ajili ya pambano la hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi dhidi ya Tanzania. Kikosi hicho kimewajumuisha nyota kadhaa wanaocheza Ligi Kuu Uingereza, Italia, Ureno na Ufaransa.

Kiungo mshambuliaji, Riyad Mahrez anayetamba na Leicester City pamoja kinda wa Totenham Hotspur Nabil Bentaleb wameitwa.

Mkali wa Porto anayezitoa udenda klabu za Ulaya, Brahimi Yassine, Sofiane Feghouli (Valencia), Slimani Islam (Sporting Lisbon) pia wamo.

Majina yote ya wachezaji: Doukha Azzedine ( JS Kabliye ),Ghoulam Faouzi ( Napoli –Italia), Riyad Mahrez (Leicester City –Uingereza ), Belfodil Ishak ( Beni Yas –UAE), Felghouli Sofiane ( Valencia – Hispania ), Brahimi Yacine ( Porto – Ureno ), Medjani Carl ( Trabzon Sport- Uturuki ), Slimani Islam ( Sportin Lisbon- Ureno ), Bentaleb Nabil ( Tottenham Hotspur – Uingereza ), Soudani Hilal El Arabi ( Dynamo Zaghreb,- Croatia ),

Wengine: Taider Sliti Saphir ( Bologna-Italia), Mandi Aissa ( Stade Reims – Ufaransa ), Kashi Ahmed ( Charlton Athletic ( Watford – Uingereza ), Zeffane Medhi Embareck ( Stade Rennes – Ufaransa ), Bounedjah Baghdad ( Etoile Du Sahel ), Mesloub Walid ( Lorrient – Ufaransa ), Boudebouda Brahimi ( USM Alger), Asselah Malik ( CR Belouizdade), Benayada Houcine ( USM Alger ),

Belkeroui Hichem ( Club African – Tunisia ), Hachoud Abderrahmen ( MC Alger ) na Khoualed Eddine wa USM Alger Wanakamilisha majina ya wachezaji 23 ambao wana asilimia kubwa ya kuwemo kwenye kikosi cha mwisho kitakachokuja Tanzania.

Wachezaji wengine kumi wanaokamilisha orodha ya kikosi cha awali ni : Mbolhi Rais ( Antalysapor – Uturuki ), Guedioura Adlane ( Watford – Uingereza ), Mesbah Eddine ( Sampdoria –Italia ), Abeid Mehdi ( Panathinaikos –Ugiriki ), Benrahma Said ( 0GC Nice – Ufaransa ), Jeaninin Mehdi ( Paris Fc-Ufaransa ), Ziti Khouthir ( JS Kabliye ), El orfi Hoocine ( USM Alger), Ghezzal Rachid ( Olympique Lyon )

Kinachoendelea ‘Kigoma Kusini’ kwa Kafulila
Hamisi Kigwangalla awakejeli Ukawa