Kocha wa Taifa Stars, Adel Amrouche ameeleza namna ambavyo kikosi chake kipo tayari kwa Mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi FC, kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) dhidi ya Uganda ‘The Cranes’, huku akiamini nyota wake watawapa raha Watanzania.

Amrouche amesema licha ya kuwa na muda mfupi wa maandalizi amefurahia uwajibikaji wa mchezaji mmoja mmoja na morali ya timu kwa ujumla, kuelekea katika mchezo huo ambao utapigwa kesho Ijumaa (Machi 24), katika Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia-Misri, kabla ya timu hizo kucheza mchezo wa Mzunguuko wanne Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Machi 28.

“Hatuna sababu ya kusingizia. Hii ni timu na tunapaswa kuwapa furaha Watanzania. Siku zote nimekuwa Kocha mwenye mtazamo chanya, hivyo naamini kuwa tunaweza kupambana na kupata matokeo mazuri kwa sababu tunao wachezaji wenye ubora na hata uzoefu,” amesema kocha huyo kutoka Algeria.

“Tumekuwa na maandalizi mazuri ambayo yamejikita kwenye mbinu juu ya namna ya kucheza na kupata matokeo. Tunapaswa kufanya kazi kwa pamoja.”

Amrouche ameongeza kuwa: “Nitafurahi kuona tunafanya vizuri kwenye michezo yote miwili dhidi ya Uganda na sote tunafahamu (Waganda) walivyo na timu ngumu na shindani,”

Katika Msimamo wa Kundi F, Taifa Stars ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 01 sawa na Uganda unayoburuza mkia wa Kundi hilo, huku Algeria ikiongoza kwa kuwa na alama 06 na Niger inafuatia kwa kuwa na alama 02.

Wachezaji Taifa Stars wala kiapo Misri
Ihefu FC yaitangulia Simba SC ASFC, Ligi Kuu