Timu ya taifa ya Argentina imeifuata timu ya taifa ya Chile katika mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya ukanda wa kusini mwa Marekani (Copa America) baada ya kuifunga Paraguay mabao 6 kwa 1 usiku wa kuamkia leo mjini Concepcion, Chile.

Mabao ya Argentina yalifungwa na winga wa Manchester United, Angel di Maria aliyefunga mawili na huku Marcos Rojo, Sergio Aguero, Javier Pastore na Gonzalo Higuain wakifunga bao moja moja kila mmoja.
Beki wa Manchester United, Marcos Rojo alianza kuifungia Argentina dakika ya 15, kabla ya Javier Pastore kufunga la pili dakika ya 27 na Lucas Barrios kuwafungia bao la kufutia machozi Paraguay kabla ya mapumziko.

Kipindi cha pili Angel di Maria akaanza ‘balaa lake’ akiifungia Argentina bao la tatu na la nne dakika ya 47 na 53, kabla ya Sergio Aguero kufunga la tano dakika ya 80 na Gonzalo Higuain la sita dakika ya 83.

Argentina watapambana na Chile July 04 kwenye uwanja wa taifa uliopo mjini Santiago na siku moja kabl ya mchezo huo Peru watapambana na Paraguay katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu.

Nike yazindua mipira ya Uingereza, Hispania na Italia Msimu Wa 2015-16
Pinda: Sitaugua Moyo Jina Langu Likikatwa