Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kiungo Jack Wilshere anatarajiwa kurejea tena dimbani majuma mawili yajayo baada ya kupata maumivu ya kifundo cha mguu.

Wilshere mwenye umri wa miaka 23, aliumia katika mazoezi ya kujiandaa na msimu wa 2015-16, ambapo ilidhaniwa huenda angekaa nje ya uwanja kwa miezi miwili.

Wenger, amesema kiungo huyo kutoka nchini England anatarajiwa kupona ndani ya muda mfupi ujao.

Wakati huo huo kiungo kutoka Jamuhuri ya Czech, Tomas Rosicky amefanyiwa upasuaji wa goti anatakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili.

Wenger alianika taarifa za wachezaji hao wawili hadharani, alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika mchezo wa pili wa ligi, ambapo mwishoni mwa juma hili The Gunners, watapambana na Crystal Palace.

Kiungo Rosicky mwenye miaka 34 aliumia mwezi juni alipokua akiitumikia timu yake ya Jamhuri ya Czech iliyomenyana na Iceland katika harakati za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016.

Ni Vita Kati Ya Stefan Effenberg Vs Hughes, Shaqir
De Gea Apasua Ukweli Wa Kuwekwa Benchi