Tanzania huzalisha takriban tani 350,000 ya mifuko ya plastiki kila mwaka na zaidi ya asilimia 70 ya taka katika Bahari ya Hindi hutokana na plastiki hali ambayo ikiendelea inaweza kuleta tatizo la ukubwa wa taka hizo kuwa nyingi zaidi katika bahari kuliko samaki na viumbe hai vingine.

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip
Mpango mara baada ya kuongoza zoezi la kufanya usafi katika soko kuu la wamachinga mjini Dodoma ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani hii leo Juni 5, 2023.

Amesema, “katika miaka michache ijayo wavuvi watakuwa wanavua maplastiki badala ya samaki. Sote tumeshashuhudia athari mbalimbali zitokanazo na taka za plastiki ambazo nimeshazisema. Kwa bahati mbaya sana, taka za plastiki haziozi haraka! Inakadiriwa kuwa mifuko ya plastiki huchukua miaka 400
mpaka 1000 kuoza.”

Aidha, Dkt. Mpango ameongeza kuwa, “tuendelee kupiga vita kwa nguvu zote matumizi ya mifuko ya plastiki na kuimarisha utunzaji wa mazingira yetu hususan bahari, maziwa na mito kwa kuepuka uchafuzi unaotokana na taka za plastiki. Nawaomba wote tukishirikiane katika hili.”

Ripoti CAG: Vipimo vyabaini baadhi ya Wanaume wana ujauzito
Kai Havertz awekewa mitego Santiago Bernabeu