Baada ya ushindi wa bao moja kwa sifuri uliopatikana jana kwenye mchezo wa mzunguuko wa tano wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Stand Utd, mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Hadji Sunday Manara alituma shukurani kwa niaba ya uongozi wa klabu hiyo kwa mashabiki na wanachama kupitia vyombo vya habari.
Aliandika:
Wanasimba wenzangu kwanza tumshukuru muumba kwa uwezo wake kutuwezesha kumaliza salama mechi yetu ya dhidi ya Stand United ya Shinyanga.
Na kwa pekee tumshukuru yeye kwa kutujaalia kupata ushindi katika game hiyo iliyokuwa ngumu.
Pia nichukue fursa hii kuwapongeza wachezaji wetu na bench Ia ufundi kwa kuweza kupambana na hatimaye kuzoa points zote tatu hii.
 
Hakika tulikuwa na mshindani halisi wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Nakiri wazi kabisa Stand United ni timu nzuri sana na wanastahili pongezi.
 
Na kama ilivyo ada shukran makhsusi ziwaendee mashabiki wetu kwa kuishangilia timu yao kwa nguvu sana na kwa wale ambao hawakuja leo uwanjani. Tunajua dua na sala zenu mlizielekeza Uwanja wa Taifa.
 
Ligi bado mbichi sana. Tusahau sasa machungu yetu ya kupoteza mechi dhidi ya watani. Maisha lazima yasonge mbele na sote tupeleke akili yetu kwenye game za mkoani Mbeya ambazo tunaujua ugumu wake.
AHSANTEN washabiki wa Simba.
Mungu ibariki Simba
Reclaiming our glory
 
Simba Nguvu Moja

 

Jurgen Klopp Aendeleza Misimamo Ya Kukataa Kazi
Nyosso Adai Kufanyiwa Hujuma