Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini ambaye pia ni Meneja wa msanii Daimond Platinum, Babu Tale ameibuka na kukanusha kuoa kama inavyosambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii.Kupitia ukurasa wake wa Instagramu Babu Tale ameandika;

“Mwenyezi Mungu (S.W) alituumba kwa upendeleo mkubwa sana, hata akaweza kumfanya Mwanadamu kuwa Kiumbe mwenye thamani kuliko hata Wanyama, Ndege na viumbe vingine.

Lengo la haya yote ni kumfanya Mwanadamu aweze kuchagua jambo lenye Kheri na Shari akiamua.

Naamini KUOA ni jambo la kheri na heshima kubwa, nami nilishafanya hivyo kwa kutambua thamani ya uumbaji wangu na faradh iliyopo kwenye Dini.

Niwe mkweli Ndugu zangu, “KIVULI CHA FARADHI KINAISHI NAMI”, hivyo najipa muda kivuli hiki kinipe nafasi. KISHA NITAOA INSHAALLAH. WAPUUZENI WAPUUZI WOTE WANAOSEMA NINAO IYO TAREHE YAO YA MITANDAONI #MALENGO.”

Mwadui FC yatangulia FDL
CHADEMA yapata mrithi wa Mdee BAWACHA