Balozi Juma Mwapachu ametangaza uamuzi wake wa kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) akibainisha kuwa chama hicho kimepoteza mueleko.

Pia, Balozi Juma ameeleza kuwa hatua hiyo inatokana na kutoridhishwa kwake na utaratibu uliotumika kuchuja majina ya makada waliotangaza nia ya kugombea nafasi ya urais kupitia chama hicho, kwamba viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho walivunja katiba.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, Balozi Mwapachu amesema kuwa atatangaza rasmi uamuzi wake kesho, Oktoba 14 ambayo ni siku maalum ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere.

Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, Balozi Mwapachu ameeleza kuwa hatajiunga na chama chochote bali ataendelea kushikilia msimamo wake wa kutokubaliana na CCM.

Balozi Mwapachu ni kada mkongwe wa CCM na alianza safari ya siasa akiwa katika chama cha TANU mwaka 1964.

Kingunge Atumia Maneno Makali Kumjibu Dkt. Bana
J Makamba Adai Magazeti ‘Hutumiwa’ Kuandika Ndivyo Sivyo Kuhusu Lowassa