Kiungo mshabuliaji wa City,Haruna Moshi Shaaban, amesema kikosi cha timu yake kina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo ujao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara ulipangwa kuchezwa jumamosi hii kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi leo asubuhi kwenye uwanja huo, Haruna ameweka wazi kuwa  City ina kikosi kilichosheheni nyota vijana wenye vipaji na uwezo mkubwa wa kucheza soka jambo linalompa imani kubwa Simba haitakuwa na nafasi ya kutamba siku ya jumamosi kwenye mchezo baina ya timu hizi.

“Nimefanya mazoezi leo kwa mara ya kwanza na kikosi changu, hakika imekuwa siku nzuri kwangu, nimegundua timu yetu ina kikosi bora, vijana wana vipaji na uwezo mkubwa wa kucheza soka, binafsi hili limenishangaza na kunipa imani kuwa Simba hawana nafasi kwetu jumamosi, tutawaadhibu”  alisema.

Haruna aliyekuwa nje ya kikosi kufuatia masuala kadhaa ya kifamilia na pia majaribio ya kucheza soka nje ya nchi  aliweka wazi kuwa amerejea kikosini kwa lengo moja tu kudhihirisha ubora wake  na pia kufanya kazi ili kuisaidia timu kupata matokeo mazuri kwenye michezo yote iliyobaki ya ligi kuu ya soka Tanzania bara.

“Nimerudi, lengo langu ni moja tu kufanya kazi kwa nguvu zote kuisaidia timu kufanya  vizuri, watu wengi wanadhana tofauti lakini muda si mrefu watakuwa na kauli nyingine juu yangu na timu yangu” alimaliza.

boban 3
Haruna Moshi (KUSHOTO) kwenye moja ya harakati zake mazoezini leo kwenye uwanja wa sokoine.

How To Write A Custom Essay Using Metaphor
Valdes Kupigwa Bei Januari 2016