Kiungo mkabaki kutoka nchini Brazil Carlos Henrique José Francisco Venâncio Casimiro, amerejea mazoezini na huenda akatumika katika mchezo wa mwishoni mwa juma lijalo kati ya Real Madrid dhidi ya FC Barcelona (El Clasico).

Casimiro amerejea mazoezini baada ya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma kadhaa, kufuatia maumivu ya kiazi cha mguu ambayo aliyapata katika mchezo dhidi ya Villareal uliochezwa septemba 22.

Hali yake kiafya imeonekana kutengemaa, na kurejea kwake katika maoezi ya kikosi cha kwanza kumeonyesha kuwafurahisha wakuu wa benchi la ufundi sambamba na mashabiki ambao wamekua wakifuatilia mazoezi ya kikosi cha klabu hiyo.

Wakati Casimiro anarejea mazoezini, Real Madrid wamepata pigo la kumpoteza mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Wales Gareth Bale ambaye atakua nje ya uwanja kwa miezi minne.

Bale aliumia kifundo cha mguu jumanne usiku akiwa katika mchezo wa mzunguuko wa tano wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Sporting Lisbon.

Taarifa zilizotolewa na klabu ya Real Madrid zimeeleza kuwa, Bale anatarajia kufanyiwa upasuaji mwanzoni mwa juma lijalo.

Pochettino: Chelsea Wana Bahati Ya Kipekee
Museveni: Ushindi wa Trump ni matokeo ya laana ya Afrika kwa Marekani