Chama tawala nchini Afrika kusini ANC kimeshindwa katika uchaguzi wa meya katika jiji la Johannesburg ambapo meya mpya wa jiji hilo Herman Mashamba anatoka chama cha upinzani cha Democratic Alliance.

Chama cha ANC kipo madarakani tangu kipindi cha ubaguzi wa rangi nchini humo zaidi ya miaka 20.

Mashamba ameahidi kubadilisha utawala wa jiji na kuahidi kutatua changamoto zinazojitokeza katika jiji hilo.Chama cha ANC kimepoteza mjimbo mengi katika uchaguzi wa mwezi uliopita ingawa bado kinaongoza nchi.

 

Wananchi Wanaoishi Karibu Na Migodi Walalamika Kulipwa Fidia Kidogo
Mamlaka Ya Bandari Yakanusha Kuwa Na Mvutano Na Wamiliki Wa Bandari Kavu Nchini