Michuano ya kabu bingwa iliendelea usiku wa jana ambapo Man Utd ikicheza ugenini nchini Urusi katika uwanja VEB Arena iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya CSKA Moscow.

Manchester United walipata mabao kupitia kwa Romelu Lukaku aliyefunga mabao mawili na mabao mengine mawili yakifungwa na Henrikh Mkhtaryan  na Anthony Matrial aliyefunga kwa mkwaju wa penati wakati  bao la CSKA Moscow likifungwa na Kuachev na kuwafanya United kuongoza kundi A.

Chelsea wameendeleza rekodi yao nzuri dhidi ya timu za Hispania ugenini baada ya hapo jana kuipiga Athletico Madrid mabao 2 kwa 1, Athletico walitangulia Chelsea kufunga kupitia kwa Antonie Griezman kabla ya Morata na Batshuayi kuifungia Chelsea mabao mawili.

Mechi kati ya Athletico Madrid na Chelsea ilikuwa mechi ya kwanza kwa Athletico kucheza katika uwanja wao mpya wa Wandra Metropolitano katika champions league.

Katika mchezo mwingine Gonzalo Higuain na Mario Mandzukic waliisaidia Juventus kupata alama 3 dhidi ya Olympiakos huku Barcelona wakipata ushindi ugenini dhidi ya Sporting baada ya goli la kujifunga la Sebastian Coates.

Polisi amuua kwa risasi mpenzi wake kisha kujiua
Chadema wamgomea Mwigulu