Wakali wa Stanford Bridge (Chelsea) wanaendelea na harakati za kutaka kumrejesha mshambuliaji kutoka nchini Ublegiji Romelu Lukaku, ambaye walikubali kumuachia mwaka 2014, na kumpeleka Goodison Park kwa dau la Pauni milioni 28.

Gazeti la Sportsmail limeripoti kuwa, Chelsea wako tayari kutoa ofa ya mchezaji Loic Remy sambamba na Pauni milioni 65 ili kufanikisha mpango huo ambao unapewa uzito mkubwa na meneja wao mpya Antonio Conte.

Hata hivyo taarifa zinadai kuwa Everton wamekubali mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, aondoke klabuni hapo, lakini kwa sharti la ada ya Pauni milioni 75 ambayo itawezesha kuvunjwa kwa mkataba wake wa miaka mitatu uliosalia.

Lakini pamoja na msisitizo huo, Everton bado hawajapokea ofa rasmi kutoka Chelsea, na pengine kikwazo ni kiasi kikubwa cha pesa kinachohitajika.

Chelsea wamemtumia Remy katika dili hilo kama mtego, kufuatia mkurugenzi wa Everton, Steve Walsh kuwahi kuonyesha nia ya kutaka kumsajili wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwaka huu.

Paul Pogba Aupa Kisogo Usajili Wa Pauni Milioni 100
Alberto Moreno Amrudisha Sokoni Jurgen Klopp