Nahodha na mshambuliaji wa mabingwa wa soka barani Ulaya “Timu ya taifa ya Ureno” Cristiano Ronaldo amekubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Real Madrid.

Taarifa za awali zilizochapishwa kwenye tovuti ya AS zinaeleza kuwa, mshambuliaji huyo atasaini mkataba wa miaka minne mpaka mitano ambao huenda ukifikia kikomo mwaka 2020 au 2021.

Ronaldo ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Real Madrid ambacho kilitwaa ubingwa wa Ulaya mwezi Mei mwaka huu, anatarajiwa kukutana na wakala wake Jorge Mendes pamoja na rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, Agosti 10, mara atakaporejea kutoka mapumzikoni.

Wakati huo huo Los Blancos, wamejipanga kumuongezea mkataba mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Wales Gareth Bale, na tayari wameshaanza kufanya vikao na wakala wake Jonathan Barnett.

Kamanda Mpinga Azindua Mkakati Kukabiliana na Ajali Barabarani
Rais amteua mkewe kuwa Makamu wa Rais