Baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kudai kuwa wamehujumiwa katika uchaguzi wa mwaka huu, Chama Cha Wananchi (CUF) kimetoa ufafanuzi wa kilichofanywa na mgombea urais wake, Maalim Seif Sharif kutangaza matokeo aliyodai aliyoyakusanya katika vituo vyote yanayoonesha akiongoza.

Akiongea na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo visiwani humo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, alieleza kuwa mgombea urais wa chama hicho hakujitangazia ushindi kama inavyodaiwa bali aliitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kumtangaza mshindi halali kwa kutumia matokeo yaliyokusanywa kwa pamoja na Tume hiyo, mawakala wa vyama pamoja wagombea.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, akifanya mahojiano na mwandishi wa habari

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, akifanya mahojiano na mwandishi wa habari

Mazrui ametoa wito kwa wananchi wote visiwani humo kuwa watulivu wakati ambapo ZEC ikisubiri watangaze matokeo rasmi. Vurugu zimeripotiwa katika maeneo mbalimbali visiwani humo ambapo polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa CUF.

Jana Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali na Waziri Kiongozi mstaafu, Vuai Nahodha waliwaambia waandishi wa habari kuwa chama chao kimefanyiwa hujuma nyingi kwenye uchaguzi wa mwaka hu.

Chameleone Amng’ang’ania Rais Museven Uchaguzi Mkuu
Kubenea Alia Na Tume, Wenje Yawemkwisha