Kocha Mkuu wa West Ham United, David Moyes anaamini atafukuzwa kazi endapo timu yake itapoteza mchezo unaofuata wa Ligi Kuu England dhidi ya Southampton utakaochezwa Jumapili (April 02).

Hata makocha waliopo kwenye benchi la ufundi wameungana na kauli ya Moyes hususan mashabiki wasipomwonyesha sapoti Moyes kuelekea mchezo huo.

Hofu imezidi kutanda ikidaiwa wakati wowote Mwenyekiti wa West Ham, David Sulliv anatatoa uwamuzi mgumu dhidi ya kocha huyo wa zamani wa Manchester United, licha ya kumkingia kifua kwa kipindi fulani.

West Ham ipo nafasi ya 18 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, katika mechi 15 za ligi imeshinda mechi mbili tu huku Moyes presha ikizidi kumpanda. Imeelezwa mwenyekiti huyo huenda akawepo uwanjani kwa ajili ya kufuatilia mechi ya ligi watakapocheza dhidi ya Southampton, huku baadhi ya mashabiki wakishinikiza mabadiliko yanatakiwa kufanyika haraka timu yao inusurike.

Moyes atazungumza na waandishi wa habari kesho kuelekea mchezo wao wa ligi, vilevile atazungumza na wachezaji wake kwaajili ya kuwapa moyo kipindi hiki kigumu ambacho wanapitia.

West Ham itacheza mechi tatu ndani ya siku saba zijazo, mechi hizo itakuwa dhidi ya Newcastle na Fulham baada ya Southampton.

Licha ya kuboronga kwenye ligi, West Ham imeonyesha kiwango bora kwenye michuano ya Europa Conference msimu huu, katika mechi 10 ilizopata ushindi kwenye michuano hiyo ina kazi ya kutoboa mchezo wake unaofuata wa robo fainali dhidi ya Gent.

Gazeti la Sportmail limefichua siri Rafa Benitez ananyemelea kazi West Ham endapo Moyes atafukuzwa kazi.

Mtibwa Sugar yatanguliza salamu Chamazi
Ushindi ni kama kunywa maji Meridianbet kasino ya mtandaoni