Mlinda mlango David de Gea, amejumuika na mashabiki wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwa mara ya kwanza baada ya taratibu za usajili wake wakuelekea Real Madrid kugoma mwishoni mwa mwezi uliopita.

De Gea alikua kimya kwa muda mrefu kupitia mtandao huo wa kijamii na hakuwahi kuandika jambo lolote kwenye ukurasa wake tangu Agust 30, hali ambayo ilizua tafrani kwa mashabiki wanaomfuata kwa kujiuliza wapi alipo mtu wao.

Hata hivyo kadhia hizo za kuulizwa mara kwa mara hazikumsukuma mlinda mlango huyo kuandika wala kuweka picha yoyote kwenye mtandao wa Twitter, ambapo wakati mwingine watu waliichukulia hali hiyo kama hasira zilizokua zikimkabili De Gea, baada ya mambo yake kuharibika siku ya mwisho ya usajili.

Wakati mashabiki wakiwa katika hali ya kujiuliza, De Gea alionekana kwa mara ya kwanza mtandaoni usiku wa kuamkia hii leo, lakini aliweka picha pekee akiwa sambamba na kiungo mshambuliaji wa Man Utd, Juan Mata pasi na kuandika jambo lolote.

Wawili hao wameonekana wakiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Hispania huko mjini Oviedo, ambapo kesho watacheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za barani Ulaya za mwaka 2016.

Mji wa Oviedo ndipo alipozaliwa Mata, na tayari baadhi ya marafiki wa De Gea amefahamu huennda alikua akidhihirisha ugeni wake kwenye mji wa rafiki yake kipenzi ambaye anachakarika naye kwenye kikosi cha Man Utd.

Mgosi: Stars Inahitaji Kumaliza Kiu Ya Wabongo
Lowassa Aiwekea CCM Mzani Kwa Wananchi