Msanii wa muziki nchini Tanzania Diamond platnumz ameamua kuitoa bure kwa Serikali hotel yake ya kisasa yenye hadhi ya nyota tatu iliyopo maeneo ya Mikocheni B isaidie katika kipindi hiki cha janga la corona kutumika kama Karantini au hospitali ya kuhudumia wagonjwa wa Corona.

Diamond amesema hoteli hiyo ameinunua siku chache zilizopita na huenda leo akaiweka mtandaoni, na wakati ikisubiria marekebisho ya kuifanya kuwa hoteli ya nyota tano ameamua kuitoa kwa Serikali wakati huu wa janga la Corona.

”Hoteli ipo maeneo ya mikocheni B ina vyumba zaidi ya thelathini, kipindi hiki kama kuna uhitaji wa karantini itumike bure na kama itafaa kutumika kama hospitali iwe rahisi zaidi kuliko watu kwenda kule mloganzila tupo radhi itumike bure kabisa” amesema Diamond.

Ameongezea kuwa janga la Corona na la watu wote hivyo ni vyema kupambana kwa pamoja kulitokomeza.

Daimond ameyasema hayo leo april 27 wakati akihojiwa kwenye redio yake ya Wasafi FM.

Mbali na msaada huo Diamond ameamua kuwalipia watanzania 500 kodi ya pango ikiwa ni sehemu ya msaada katika kujali wale wote wanaopitia wakati mgumu kipesa kufuatia janga hili la corona ambapo amesema atatoa kodi hiyo kwa miezi mitatu mikoa yote nchini.

Serikali yaingilia kati hatma Maghorofa yaliojaa maji Mbweni
Watanzania kupata injili kwa SMS mtandao kipindi cha Corona

Comments

comments