Serikali imeteua mkoa wa Dodoma kuwa mwenyeji wa sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara yatakayofanyika Desemba 9, katika uwanja wa Jamhuri.

Uongozi wa mkoa wa Dodoma umeunda kamati ya maandalizi kwa ajili ya sherehe hizo, huku ukisema kuwa kila kitu kimeshakamilika.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema kuwa maonyesho hayo yatapambwa na gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama nchini.

Aidha, katika maonyesho hayo, kutakuwa na gwaride la mkoloni ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kufanyika tangu kuanzishwa kwake.

Hata hivyo, Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Uhuru wetu ni tunu, tuudumishe, tulinde rasilimali zetu, tuwe wazalendo, tukemee rushwa na uzembe.

 

Video: Hatma Dk. Shika mikononi mwa DPP, Waziri wa JK aeleza machungu ya kulala selo tatu Polisi
TAKUKURU yapanga mikakati mipya