Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi amefanikiwa kupata tuzo nchini Uganda kutokana na kiwango alichokionyesha msimu uliopita alipokuwa akicheza soka nchini humo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Okwi ameweka picha akiwa na tuzo hiyo ya Mchezaji Aliyependwa na Mashabiki wa Uganda, kisha akaandika:

“Napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote kwa zawadi hii na kwa kuendelea kuniunga mkono katika maisha yangu yote ya soka. Nawashukuru FUFA kwa kuwezesha hili kuwezekana.”

Okwi amepata tuzo hiyo kutokana na kiwango kizuri alichokionyesha wakati akiichezea SC Villa ya Uganda ambapo tuzo yake alikabidhiwa na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA), President Darius Mugoye.

Tuzo hizo zilitolewa wikiendi iliyopita, Okwi alikuwa nchini humo kutokana na kuwa majeruhi huku Ligi Kuu ya Vodacom ya Tanzania Bara ikiwa imesimama kwa muda.

Aidha, Okwi aliongeza kuwa anashukuru kwa tuzo hiyo ambapo alipeleka shukrani zake nyingi kwa wachezaji wa SC Villa na mashabiki wao.

Tuzo hiyo iliambatana na fedha shilingi milioni moja ya Uganda.

Mbaraka Yusuf kuwakosa Zanzibar Heroes
Kili Stars yajifua, Ninje akubali