Mshambuliaji wa Tanzania Bara, Mbaraka Yusuf Abeid hataweza kucheza mechi ijayo ya Kundi A Kombe la Challenge dhidi ya Zanzibar Desemba 7, mwaka huu baada ya jana kushindwa kufanya mazoezi kutokana na maumivu ya misuli.

Hayo yamethibitishwa na kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Ammy Conrad Ninje alipozungumza na Waandishi wa Habari nchini Kenya ambako michuano ya Challenge inafanyika mwaka huu.

Mbarak Yusuf ndiye mchezaji pekee ambaye hakufanya mazoezi jana baada ya kuumia misuli kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi A juzi dhidi ya Libya timu zikitoka sare ya 0-0.

Baada ya sare ya 0-0 na Libya juzi, Kilimanjaro Stars itarudi uwanjani keshokutwa kumenyana na ndugu zao, Zanzibar kabla ya Desemba 9 kucheza na Rwanda na Desemba 11 kukamilisha mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na wenyeji, Kenya.

 

Kilimanjaro Stars ipo kundi A pamoja na timu za Zanzibar, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.

 

Zanzibar Heroes yafanya kufuru Kenya
Emmanuel Okwi mchezaji bora Uganda