Mabingwa wa soka nchini Ujerumani, FC Bayern Munich wamepiga hodi katika klabu ya Villareal kwa ajili ya kumsajili kiungo Victor Ruiz.

The Bavarians, wameweka nia ya kutaka kusuka kikosi bora cha msimu ujao kitakachopambana kwa ajili ya mataji ya ndani na nje.

Bosi wa Bayern, Pep Guardiola amenukuliwa akisema anamwania kiungo huyo raia wa Hispania kwa sababu anatambua mchango wa wachezaji wa kiwango chake.

“Nina uhakika wa wachezaji wanaocheza katika La Liga kwasababu ni Ligi ya mchakamchaka inayofanana na Bundesliga.” “Victor Ruiz ni aina ya wachezaji ambao wanaweza kucheza katika Ligi yoyote kutokana na umri wake na hata aina ya kiwango alichonacho,” alisema Guardiola.

Aliongeza: “Vitor Ruiza alikuwa ni chaguo langu, kama mambo yataonyesha kukwama nitaangalia namna ya kumsainisha kiungo huyo mapema iwezekanavyo.”

Mabingwa hao watetezi wa Ujerumani wameweka nia hiyo baada ya kuridhishwa na kiwango cha kiungo huyo aliyezaliwamwaka 1989.

Victor aliingia katika mpango wa Bayern katika usajili wa dirisha dogo la mwezi Januari, mwaka huu, lakini sasa wanamwinda kwa udi na uvumba.

Bosi wa Bayern, Pep Guardiola amenukuliwa akisema anamwania kiungo huyo kwasababu anatambua mchango wa wachezaji wanaocheza Ligi ya La Liga.

 

Van Gaal Aanza Mbwembwe Baada Ya Kuifunga Liverpool
Real Madrid Kuwasilisha Rufaa FIFA