Floyd Mayweather amesema kuwa amepewa fedha chungu nzima ili kumshawishi arudi katika ulingo wa ndondi.

Licha ya kupewa fedha hizo ,Mayweather ambaye alistaafu baada ya pigano lake la 49 mnamo mwezi Septemba hana mpango wa kurudi ulingoni.

”Kwa sasa hivi ,nimeamua kustaafu kabisa”,alisema bingwa huyo mwenye umri wa miaka 38.

”Iwapo nitahisi kurudi,haitakuwa sababu ya kutaka fedha”,lakini ni lazima nilipwe,hiyo ndio maana ya jina lango Money Mayweather”.

Mayweather ameshinda mataji ya dunia katika mizani mitano tofauti kabla ya kustaafu na rekodi nzuri.

Yuko katika harakati za kuanza ziara yake ya Uingereza ambapo atazungumza na BBC Michezo kuhusu mambo anayofanya kwa sasa.

Mayweather akizichapa na Manny Paqcuiao

Mayweather alimshinda Manny Pacquiao katika pigano lililoangaliwa na wengi katika historia na amepinga kupigana tena na Manny Pacquiao.

Tamko hilo linajiri licha ya Michael Koncz,mshauri wa kibiashara wa Pacquiao kusema kwamba wanawasiliana na kampuni ya Mayweather Promotion kuhusu uwezekano wa pigano hilo.

”Maneno yoyote ambayo mumesikia kutoka kwa Michael Koncz na Bob Arum ni ya uwongo.Nimezungumza na Bob Arum na Michael Koncz”.

Neymar Kumaliza Mzizi Wa Fitna Kizimbani
Klopp: Liverpool Jengeni Imani Na Maamuzi Yangu