Kocha wa muda wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate, ametamba kuwa mtu aliyerejesha nidhamu ya kimcheza katika kikosi cha timu hiyo, ambayo mara kadhaa imekua ikishindwa kufikia malengo katika michezo ya michuano mbali mbali duniani.

Southgate aliwaambia waandishi wa habari kuwa, anaamini amefanikisha hali ya nidhamu ya kimchezao kwa wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa tangu alipoteuliwa kuchukua majukumu ya kuliongoza benchi la ufundi kwa muda, baada ya kujiuzulu kwa Big Sam mwezi Septemba.

Tambo za kocha huyo zimekuja kufuatia matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili iliyopatikana katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya England dhidi ya mabingwa wa dunia wa mwaka 2010, timu ya taifa ya Hispania usiku wa kuamkia hii leo.

Katika mchezo huo England walitangulia kupata mabao mawili ya kuongoza kupitia kwa Adam Lallana na Jamie Vardy katika dakika ya 9 na 48, lakini Hispania walisawazisha kwa mabao yaliyofungwa na Lago Aspas na Isco dakika ya 89 na 90.

“Sina budi kusema kuna mabadiliko makubwa ambayo yameonekana katika kikosi cha England, naamini umoja na ushirikiano wa wachezaji ndio chanzo cha yote haya,

“Inalazimika kwa wachezaji kupewa sifa ya kipekee kwa sababu walionyesha uwezo mzuri japo tulikubali kufungwa mabao katika dakika za mwisho, lakini ukomavu wa kiushindani umeonekana.” Alisema Southgate.

Kocha huyo wa muda tayari ameshaiongoza England katika michezo mitatu ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, ambapo alishinda dhidi ya Malta na Scotland huku akipata matokeo ya sare mbele ya Slovenia.

Matokeo ya michezo mingine ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo.

Nepal 1 – 0 Macau

Kenya 1 – 0 Liberia

Gabon 1 – 1 Comoros

Tunisia 0 – 0 Mauritania

Bahrain 0 – 0 Kyrgyzstan

Jordan 0 – 0 Lebanon

Russia 1 – 0 Romania

Msumbiji 1 – 1 Afrika kusini

Malta 0 – 2 Iceland

Hungary 0 – 2 Sweden

Ukraine 2 – 0 Serbia

Jamuhuri ya Czech 1 – 1 Denmark

Austria 0 – 0 Slovakia

Italia 0 – 0 Ujerumani

Ufaransa 0 – 0 Ivory Coast

Ireland ya kaskazini 0 – 3 Croatia

Morocco 2 – 1 Togo

Argentina Yapoza Machungu, Yaitandika Colombia
Serikali yafafanua matumizi michango ya waathirika wa Tetemeko Kagera