Kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Ya Kongo, Youssouf Mulumbu ataikosa michezo ya awali ya msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza kufuatia majeraha yanayomkabili kwa sasa.

Mulumbu atakishuhudia kikosi cha klabu yake ya Norwich City kikianza kampeni ya kuwania ubingwa wa Uingereza mwishoni mwa juma hili, baada ya kubainika amevunjika mfupa wa kidole cha mguu uitwao metatarsal.

Mulumbu alipatwa na majeraha hayo akiwa katika mchezo wa kujiandaa na msimu mpya, ambapo Norwich City walipambana na Brentford mwishoni mwa juma lililopita.

Meneja wa klabu ya Norwich City, Alex Neil jana alipokutana na waandishi wa habari, alithibitisha kuumia kwa kiungo huyo aliemsajili katika kipindi hiki baada ya kupokea taarifa za matokeo ya vipimo alivyofanyiwa.

Hata hivyo Neil amesema kutokuwepo kwa Mulumbu mwenye umri wa miaka 28 katika michezo kadhaa ya mwanzo, hakutoathiri mipango yake kufanya yaliyowapelekea katika ligi kuu ya soka nchini England.

Mulumbu alisajiliwa na The Canaries, baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya West Brom mwishoni mwa msimu wa 2014-15.

Norwich City wataanza mchakato wa kuwania ubingwa wa nchini England kwa kucheza na Crystal Palace

 

Arsenal Kumkosa Wilshere Kwa Majuma Kadhaa
Juventus Wamkaushia Oscer