Mwanamitindo, Hamisa Mobeto amefunguka kuhusu kilichopo kati yake na Boss wa WCB, Diamond Platinumz baada ya tetesi kusambaa kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi uliofichika.

Mrembo huyo ambaye amekuwa akivunja mitandao ya kijamii kutokana na yale yanayosemwa kuhusu yeye na Diamond, amesema kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wa mapenzi na mwimbaji huyo na hata hawako karibu.

“Hiyo siyo kweli hata kidogo. Badala yake, sijawahi kuwa karibu sana na Diamond na kwa mara ya kwanza tunakutana ilikuwa wakati anazindua video ya Number One pale Serena,” Hamisa aliliambia gazeti moja la Kiingereza nchini. “Actually, wakati hiyo story inaanza kusambazwa mimi nilikuwa nje ya nchi,” aliongeza.

Hata hivyo, majibu ya mrembo huyo yameacha maswali zaidi kwani hivi karibuni amekuwa akionekana kwenye matukio kadhaa ya Diamond akiwa karibu na ndugu wa msanii huyo.

Haijulikani wazi kama anayemualika kwenye matukio hayo muhimu ni Diamond ama ni ndugu zake wa karibu. Hivi karibuni, Hamisa alidaiwa kusafiri na Diamond kwenda Mbeya ambapo msanii huyo alikuwa na show, na walipanda ndege moja kwenda na kurudi.

Hamisa Mobeto

Hamisa ni mama wa mtoto mmoja, tetesi zinazovuma zinamtaja mrembo huyu kuwa tishio kwa uhusiano wa mrembo wa Uganda ambaye ni mama mtoto wa Diamond, Zari the Bosslady.

Jeshi la Polisi latolea majibu picha za askari wakifanya mazoezi
Dawasco Kanda Ya Tabata Yaendelea Kutoa Vifaa Kwa Wateja wake