Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa idara zote za serikali kutumia kiwanda cha uchapishaji cha Stardand Printer kinachomilikiwa na kampuni ya gazeti la serikali TSN

Amesema hayo baada ya kutembelea kiwanda hicho ambapo ameeleza mafanikio ya kuwepo kwa kiwanda hicho yanatokana na uthubutu wa uongozi wa kampuni.

Kiwanda hiki kinaiwezesha TSN ambayo awali ilitegemea serikali kuu kwa asilimia 100 kujitegemea kimapato, miradi kama hii inatupeleka kwenye mifumo mipya ya kujiendesha kibiashara ninazihamasisha idara zote za serikali zenye kazi ya kuchapisha zije TSN kuna mtambo wa kisasa” amesema Waziri Mwakyembe

Amesema kuwa matokeo hayo ni muendelezo wa mambo makubwa ambayo serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli imeendelea kuyafanya amesisitiza kuwa kiwanda hicho kinaiwezesha taaasisi kujitegemea kimapato.

Halikadhalika Dkt. Mwakyembe ameipongeza kampuni hiyo kwa kuwa imethubutu kuanza kusambaza magazeti yake nje ya nchi hasa nchi za Afrika Mashariki hatua ambayo imesaidia kusambaza kiswahili kwa kiasi kikubwa.

Fraga: Puuzieni mitandao ya kijamii, bado nipo Simba SC
Juma Abdul kuvuka Mpaka