Klabu ya Everton imemsajili kiungo kutoka nchini Senegal Idrissa Gueye akitokea Aston Villa kwa ada ya Pauni milioni 7.1.

Gueye, mwenye umri wa miaka 26 amekamilisha dili la usajili wa kuelekea Goodison Park kwa kukubali kusaini mkataba wa miaka mitano.

Meneja mpya wa Everton, Ronald Komen amefanikisha usajili wa kiungo huyo ambaye ameshaitumikia timu yake ya taifa ya Senegal katika michezo 32, kufuatia kuridhishwa na uwezo wake tangu akiwa Aston Villa.

Kwa mara ya kwanza Guaye alicheza katika ligi ya nchini England mwaka mmoja uliopita baada ya kusajiliwa na Aston Villa akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Lille kwa ada ya Pauni milioni 9.

Tayari Koeman ameshamsajili mlinda mlango kutoka klabu ya Fulham Maarten Stekelenburg lakini yupo kwenye hatari ya kumpoteza beki kutoka nchini England John Stones anaewaniwa na Man City kwa dau la Pauni milioni 50, sambamba na mshambuliaji kutoka Ubelgiji Romelu Lukaku, ambaye yu njiani kurejea Chelsea kwa ada ya usajili ya Pauni milioni 70.

Swansea City Wapingana Na Ashley Williams
Video: Basata wakanusha kumalizana na Msanii Nay wa Mitego