Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli leo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu kuhusu mkutano huo, Jaji Lubuva amemhakikishia Rais Magufuli kuwa NEC iko huru na haijawahi kuingiliwa katika maamuzi yake na Rais au kiongozi yeyote.

Jaji Lubuva amemueleza Rais Magufuli kuwa Tume ya Uchaguzi inapaswa kuwa huru na kwamba hilo limekuwa likifanyika wakati wote hapa nchini.

Akizungumzia mzozo wa uchaguzi visiwani Zanzibar, Jaji Lubuva alieleza kuwa Rais hana mamlaka ya kikatiba kuingilia maamuzi ya Tume ya uchaguzi visiwani Zinzibar hata bara.

“Unaposikia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano aingilie hilo suala la uchaguzi wa Zanzibar, yeye kwa kweli hana mamlaka kabisa. Pili ni kama kujikanganya, huku unasema tuwe na tume huru isiyoingiliwa halafu huku unasema aingilie kati maamuzi ya tume” alisema Jaji Lubuva.

Aidha, Jaji Lubuva aliwasihi watanzania kuwa uchaguzi umekwisha hivyo waungane na viongozi waliochaguliwa kuleta maendeleo.

Katika hatua nyingine, Jaji Lubuva amempa Rais Magufuli taarifa kuhusu kikao cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika jijini Kampala Uganda kilichojadili Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika Tarehe 18 mwezi huu.

Ray C awaka baada ya kudaiwa amekutwa kwenye chimbo la Dawa za kulevya
TFF Yaipongeza Ruvu Shooting