Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Jamal Katundu, ametoa wito kwa jamii kuwakumbuka na kuwajali watu wenye ulemavu ambapo amesema kundi hilo lina nafasi muhimu katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Ametoa wito, aliposhiriki chakula cha mchana na jamii ya wanafunzi na watumishi wa Chuo cha Ufundi Stadi kwa watu wenye ulemavu Yombo cha jijini Dar es Salaam katika kusherekea sikukuu ya Idd el Fitr.

“Nitoe wito kwa jamii kwa ujumla kutenga muda wao kwa ajili kujumuika na watu wenye ulemavu ili kuendelea kuwapa faraja na kuwatia moyo wa kuendelea kujituma na kutoa mchango wao katika ujenzi wa Taifa letu kwa kadri inavyowezekana,” alisema Prof. Katundu na kuongeza

“Kwa upande wetu sisi kama serikali tunaendelea kutimiza wajibu wetu wa kuwahudumia Watanzania wote bila kujali hali zao na ndio maana leo tumeona ni vema kujumuika na vijana wetu wenye ulemavu ambao wanapatiwa mafunzo katika chuo hiki ambacho ni miongoni mwa vyuo vyetu vilivyopo katika kanda mbali mbali kwa ajili ya kuwalea na kuwapa ujuzi vijana wenye ulemavu wa aina tofauti ikiwemo uziwi, ulemavu wa ngozi, ulemavu wa viungo nakadhalika.”

Katibu Mkuu huyo amesema serikali imeanza kufanya maboresho ya miundombinu katika vyuo vya ufundi vya watu wenye ulemavu nchini ili kuliwezesha kundi hilo maalum kupata ujuzi muhimu utakaoliwezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli mbali mbali za uzalishaji mali.

Wanawake elfu 30 wanapata Fistula nchini Tanzania kila mwaka
Viongozi wa Afrika watakiwa kushirikian na vyombo vya habari