Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambaye yuko katika riadha ya kisiasa ya kutafuta ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kumkabidhi kijiti cha kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekitaka chama hicho kumpitisha kiongozi kijana atakayesimamia vyema mawazo ya kizazi kipya.

Makamba ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa Singida akikusanya sahihi za wanachama wa chama hicho wenye nia ya kumdhamini kuwania urais mwezi Oktoba mwaka huu.

Alisema wazee wameiongoza vizuri nchi hii tangu miaka ya 1960 lakini sasa ni muda wa kuwapa nafasi vijana ili walete mabadiliko ambayo watanzania wanayahitaji.

Alisisitiza kuwa watanzania wanahitaji mabadiliko na wasiopoyaona watayatafuta sehemu nyingine wanapodhani watayapata.

January Makamba ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bumbuli, alipata wadhamini 8,300 mjini humo. Leo mbunge huyo yuko jijini Arusha akiiweka mbele kauli mbiu yake inayoonesha jinsi anavyopanga kuleta mabadiliko, ‘Tanzania Mpya’.

Kocha Mkongwe Akubalia Kuachia Ngazi Uholanzi
Jarida la SA hip hop lamtaja Fid Q kati ya rapaz bora 20 Afrika