Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba anamuona waziri wa kazi, John Pombe Magufuli kama chaguo sahihi la CCM litakaloirudisha imani ya wananchi kwa chama hicho.

Kupitia Instagram, Makamba ameonesha kumuunga mkono kwa asilimia zote John Pombe Magufuli kama walivyofanya baadhi ya wagombea waliokuwa kwenye kinyang’anyiro cha kuchaguliwa katika nafasi ya kuipeperusha bendera ya CCM kuwania kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Mchakato wa kumpata Mgombea wa Chama chetu umekamilika. Nampongeza kwa dhati Ndugu John Pombe Magufuli kwa kupata heshima ya kukiwakilisha Chama chetu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu kwa nafasi ya Urais. Naamini atarejesha imani ya wananchi kwa Chama chetu. Sina shaka atainadi vyema Ilani ya Chama chetu na kutupatia ushindi wa kishindo pamoja na kuunda Serikali itakayoakisi matarajio ya Watanzania walio wengi. Jukumu letu wana-CCM wote ni kumnadi kwa nguvu moja.
Nawashukuru wote kwa pongezi zenu za Tano Bora. Nawashukuru wale wote mlioonyesha imani yenu kwangu tangu mwanzo na wengine wote mliotuunga mkono. Mlitupa nguvu. Nawashukuru pia mliotupinga na kutukosoa. Mlitusaidia kujitazama na kujirekebisha.”

Mchakato wa kumpata Mgombea wa Chama chetu umekamilika. Nampongeza kwa dhati Ndugu John Pombe Magufuli kwa kupata heshima ya kukiwakilisha Chama chetu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu kwa nafasi ya Urais. Naamini atarejesha imani ya wananchi kwa Chama chetu. Sina shaka atainadi vyema Ilani ya Chama chetu na kutupatia ushindi wa kishindo pamoja na kuunda Serikali itakayoakisi matarajio ya Watanzania walio wengi. Jukumu letu wana-CCM wote ni kumnadi kwa nguvu moja. Nawashukuru wote kwa pongezi zenu za Tano Bora. Nawashukuru wale wote mlioonyesha imani yenu kwangu tangu mwanzo na wengine wote mliotuunga mkono. Mlitupa nguvu. Nawashukuru pia mliotupinga na kutukosoa. Mlitusaidia kujitazama na kujirekebisha.

A photo posted by January Makamba (@jmakamba2015) on

UKAWA Wataja Tarehe Ya Kumtangaza Mgombea Wa Urais
Audio: Drake Ashiriki Kwenye Remix Ya Ojuelegba Ya Wizkid