Jogoo anayefahamika kwa jina la Maurice ameshinda kesi nchini Ufaransa ambapo mahakama imewaamuru walalamikaji ambao ni wanandoa, Jean Loius Biron na Joell Andrieux kumlipa mmiliki wa jogoo huyo, Crinne Fesseau  shilingi za kitanzania milioni mbili na nusu kwa usumbufu.

Jogoo huyo kutoka kisiwa cha Oleron katika pwani ya Atlantic alifunguliwa shtaka kwa kuwakera na kuwasumbua wanandoa waliostaafu wanaomiliki nyumba ya likizo katika eneo hilo hivyo  kutokana na kelele za jogoo huyo kila asubuhi waliamua kumfungulia kesi wakidai kuwa amekuwa akiwasumbua tangu mwaka 2017 kwa kuwika kila asubuhi.

Ni ushindi wa kila mtu aliyepo katika hali yangu natumai uamuzi huo utakuwa wa kuigwa, Crinne Fesseau alinukuliwa na gazeti la AFP.

Wakati wa kusikiliza kesi hiyo mwezi Julai, mawakili wa jogoo huyo walihoji kwamba malalamishi hayo ni hafifu kwa kuwa kuwika kwa jogoo huyo ni hali ya kawaida ya maisha ya taifa hilo.

Kesi hiyo iliungwa mkono na watu 140,000 katika mitandao ya kijamii waliowasilisha ombi la kuipinga.

Hii ni moja ya kesi iliyopata umaarufu na kuzua wasiwasi mkubwa kati ya wakazi wanaoishi mashamabani nchini Ufaransa na wale wanaohamia mashambani ili kutoroka mjini.

Aidha, Meya wa mji mwingine, Bruno Dionis du Sejour aliandika katika barua ya wazi mnamo mwezi mei akitaka kelele za maisha ya vijijini ikiwemo zile za ng’ombe na kengele za makanisani ziandikwe kwenye orodha ya urithi wa Ufaransa ili kuwalinda dhidi ya malalamishi kama hayo.

Video: Safari ya Biashara Tanzania na Uganda yaanza kwa sura Mpya
Eto'o 'Baharia' aliyetia nanga baada ya miaka 23