Kada wa CCM ameelezea kile alichokiita mkakati unaosukwa ndani ya chama hicho kuliondoa jina la waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenye mchakato wa kuyapata majina matano yatakayotangazwa muda wowote mjini Dodoma .

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, chanzo hicho kilichopo mjini Dodoma kililieleza gazeti hilo kuwa uongozi wa juu wa chama hicho ulimuagiza jaji mmoja ambaye jina lake halikuwekwa wazi kuandika waraka mzito kuonesha kuwa Lowassa alikiuka sheria ya uchaguzi.

“Huwezi amini, kuna jaji mmoja amepewa kazi9 ya kuandika waraka mzito na kuupeleka Kamati ya Maadili na baadaye Kamati Kuu, eit Lowassa amekiuka Sheria ya Uchaguzi,”Mtanzania imekinukuu chanzo hicho.

“Tumeshangazwa mno na hatua hiii, ndiyo maana kwa siku mbili mfululizo Kamati ya Maadili na Kamati Kuu zimeshindwa kukaa kwa sababu wanasubiri waraka wa jaji huyo,” kiliongeza chanzo hicho.

Hata hivyo, mambo yanayendelea ndani ya vikao vikuu vya chama hicho mjini Dodoma yanafanyika kwa siri kubwa huku vyombo vya habari vikiambulia taarifa chache za ratiba na kinachoendelea nje ya kikao hicho. Mengi yanayozungumzwa na wapambe wa wagombea yametafsiriwa kuwa sehemu ya upepo wa presha ya kuyapokea matokeo.

R. Kelly Ashitakiwa Na Kaka Yake Wa Damu Kwa Dhuruma
Majina Matano Mbele Ya NEC Leo