Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Kassim Dewji amethibitisha kuachia nafasi hiyo, ikiwa ni siku chache baada ya kupatikana kwa wajumbe wa Bodi hiyo upande wa Wanachama.

Kassim ambaye amewahi kuhudumu nafasi mbalimbali za uongozi klabuni hapo kwa miaka 34, amekuwa Mjumbe wa Bodi hiyo kwa zaidi ya miaka minne upande wa Mwekezaji Mohamed Dewji ‘Mo’.

Mdau huyo ameandika Barua na kuianika hadharani ikieleza sababu za Kibiashara na Familia, ndizo zilizomsukuma kujiuzulu nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC.

“Nitastaafu ngazi zote za kuteuliwa au kuchaguliwa, nimekuwa katika famialia ya Simba kwa muda mrefu tangu mwaka 1989, nimefurahi mafanikio mengi katika kipindi hicho, nimefanikiwa kuwaandaa viongozi mbalimbali katika nyadhifa tofauti.”

“Ni wakati muafaka sisi wazee tupumzike katika nafasi za uendeshaji na maamuzi katika klabu yetu pendwa.” imeeleza sehemu ya Barua ya Kasim Dewji iliopelekwa kwa Mwenyekiti.

Tetemeko la ardhi Uturuki, Watanzania wapo salama: Balozi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 7, 2023