Rapper wa kike wa Uganda, Jocelyne Tracey maarufu kama Keko, amejikuta akikitia kitumbua chake mchanga na kufukuzwa kwenye kipindi cha Coke Studio Afrika kinachowakutanisha wasanii wakubwa Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo, Keko alifanya vurugu katika chumba cha hotel maeneo ya Southern Sun Maifair ambapo uongozi wa hotel hiyo ulishindwa kumvumilia na kumtimua.

Chanzo kutoka hotelini hapo kilieleza kuwa mkali huyo wa ‘Make U Dance’ hakuwa na mtu wa kumsaidia na baadae alionekana akiwa katika eneo la parking la kituo cha mafuta.

Baada ya tukio hilo alipelekwa hospitali kupata matibabu kabla ya kurudishwa kwao Uganda.
Nafasi yake katika coke studio afrika imechukuliwa na Navio wa uganda.

Lulu Kuachia Filamu Mpya ‘Ni Noma’ Aliyoipika Mwaka Mzima
Kardashians Waendelea Kumtonesha Amber Rose Madonda ya Mapenzi