Matukio mengi yanazidi kuongezeka zikiwa zimebaki siku 25 tu kabla watanzania hawajapiga kura kumchagua rais wa awamu ya tano,  mengine yakiwa ya kufurahisha, mengine ya kuudhi lakini mengine ya kusikitishwa.

Mgombea urais wa Chadema anaeungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa ameelezwa kusikitishwa na tukio la polisi kuwapiga mabomu wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakitoka katika uwanja wa Tangamano jijini Tanga.

Lowassa ameeleza kusikitishwa kwake na tukio hilo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi katika uwanja wa Chuo Cha Ualimu, Korongwe, Tanga.

“Niliporejea hotelini baada ya mkutano wa jana, nilipata taarifa kuwa polisi waliwapiga mabomu wafuasi wa Ukawa, nasikitika sana kwa kitendo kil, kwa sababu tulikubaliana polisi wasipige watu mabomu,” alisema Lowassa.

Mgombea huyo aliwataka polisi kutowapiga mabomu wananchi bali washirikiane nao ili wafanye kazi pamoja.

Lowassa ambaye aliwaahidi wananchi hao kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais wa Tanzania, ataifumua Bandari ya Tanga na kuijenga upya pamoja kufufua reli mkoani humo.

‘Ukawa Wana Uhakika Wa Kushindwa, Wameshakata Tamaa’
Ndikumana Amuhurumia Nyosso