Bingwa wa dunia uzani wa juu, Wladimir Klitschko amempiga kijembe mpinzani wake Tyson Fury kwa kumwambia amekua na tabia ya kuzungumza sana katika vyombo vya habari kuliko matendo yake anapokua ulingoni.

Klitschko mwenye umri wa miaka 39 anatarajia kupambana na mpinzani wake Oktoba 24 mwaka huu, huku dunia ikimtambua kama mmiliki wa mikanda ya ubingwa duniani ya WBA, WBO, IBF pamoja na IBO. Bondia huyo amesema yupo tayari kuendeleza ubabe wake.

Wawili hao watapambana nchini Ujerumani katika uwanja wa Esprit Arena, wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 54,600 walioketi.

Klitschko amesema anaendelea kujiandaa kikamilifu katika kipindi hiki, na lengo lake ni kutaka kuuonyesha ulimwengu kuwa bado ana uwezo wa kuwanyamazisha wapinzani wake hususan wanaotoka Uingereza, kwa kusisistiza mabondia wanaotoka nchini humo wanazungumza sana kupitia vyombo vya habari kuliko vitendo.

Tayari Klitschko, alishapambana na bondia kutoka Uingereza mwaka 2011, David Haye na alifanikiwa kumshinda kwa points.
Wakati huo huo bondia Tyson Fury mwenye umri wa miaka 26, amemjibu mpinzani wake kupitia picha aliyoiweka kwenye mitandao ya kijamii ambayo inamuonyesha akiwa ameziba mdomo wake kwa Plasta.

Picha hiyo imemaanisha Fury hana tabia za kuzungumza zungumza sana zaidi ya kusubiri vitendo ulingoni.

Tailor Swift Asaidia Kuokoa Maisha Ya Mtoto Anaeteswa Na Leukemia
Singida Mjini Wamlilia Mo Dewji Baada Ya Kujiengua Ubunge