Mwanasheria Mkuu wa Chadema ambayo ni moja kati ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Tundu Lissu alijibu moja kati ya maswali ambayo waanzania wengi wamekuwa wakijiuliza katika mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Wananchi wengi wamekuwa wakihoji sababu za Ukawa hususan Chadema kuiacha ajenda ya kupambana na ufisadi waliyoihubiri sana katika kampeni za mwaka 2010.

Kwa mujibu wa Tundu Lissu, mahubiri hayo ya ufisadi yameshahubiriwa sana kwa muda mrefu hivyo wananchi wanataka kusikia mambo mengine yanayowaletea maendeleo.

“Kwa sasa neno ufisadi halijitokezi sana kwa sabsabu tumezungumza ufisadi kwa zaidi ya miaka kumi na watanzania wameelewa msimamo wetu,” alisema. “Tunahitaji kupanua ajenda yetu na hatuwezi tukagombea uchaguzi wa urais kwenye eneo moja tu la ufisadi. Ni lazima tupanue wigo wa masuala yanayowakabili wananchi.”

Ukimya wa Ukawa juu ya ufisadi unahusianishwa na uamuzi wa chama hicho kumpa Edward Lowassa nafasi ya kugombea urais, miaka mitano michache baada ya kumtaja katika orodha ya mafisadi.

Ajenda ya ufisadi hivi sasa imeonekana kutumiwa zaidi na upande wa CCM ambao haukuwa na ajenda hiyo mwaka 2010. Mgombea wa CCM, Dk John Magufuli ameendelae kuchanja mbuga kwa msimamo wake wa kupambana na ufisadi nchini huku akiahidi kufungua mahakama maalum ya ufisadi.

CCM Wamsakama Maalim Seif
Malinzi Azindua Kambi Ya U13 Mwanza