Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kuwa uamuzi aliouchukua, Lazaro Nyalandu wa kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni kitendo cha ujasiri mkubwa.

Lissu ambaye anatibiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya baada ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana alimtumia salamu hizo za pongezi, huku akiwataka wapiga kura katika uchaguzi mdogo wa madiwani kuchagua chama chake.

“Nimepokea kwa faraja kubwa kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge jirani yangu Jimbo la Singida Kaskazini, Mheshimiwa Lazaro Nyalandu kutoka CCM na kuomba kujiunga Chadema, ameitumikia CCM karibu miaka 20, leo kaamua kujiunga na Chadema ni uamuzi sahihi,”amesema Lissu

Aidha, Nyalandu amekuwa ni baadhi ya wabunge wachache ambao wamekuwa wakienda mara kwa mara jijini Nairobi nchini Kenya kumjulia hali mbunge huyo wa chadema aliyelazwa kwaajili ya matibabu.

Hata hivyo, wabunge mbalimbali wa Chadema kupitia akaunti zao za kijamii wameonyesha kufurahishwa na uamuzi wa Nyalandu wa kuamua kuondoka CCM na kuomba kujiunga Chadema.

Baada ya miaka minne Man Utd yapiga hatua Champions League
Video: Lissu 'Karibu Nyalandu', Meya mwenye siri nzito amtaka Magufuli faragha