Majogoo wa Jiji Liverpool wana nafasi kubwa ya kumsajili kiungo wa kimataifa wa Argentina Alexis MacAllister anayekipiga klabu ya Brighton, huku ikielezwa kila kitu kipo sawa na sasa ni suala kwa mchezaji huyo kutua Anfield.

Liverpool imeshafikia makubaliano ya kumsajili mchezaji huyo ambaye yeye mwenyewe ameonesha nia ya kujiunga na klabu hiyo.

Hadi sasa majogoo wa Anfield wameshakubaliana maslahi binafsi na MacAllister kilichobakia ni kulipa ada ya uhamisho kwa Brighton.

Dalili za kiungo MacAllister kuondoka ndani ya Brighton zilionekana pale ambapo kocha wa klabu hiyo, Roberto de Zerbi aliposema kuwa inawezekana akawakosa wachezaji wake muhimu ndani ya msimu ujao.

Huku majina kama MacAllister na Moises Caicedo yakiwa yametajwa kuwa wanaachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Liverpool inaelezwa inataka kuharakisha zaidi nafasi ya kiungo na walikuwa wa kwanza kumwania MacAllister ambaye alikuwa akiwindwa na Manchester United.

MacAllister amekuwa na msimu bora ndani ya Brighton pamoja na timu ya taifa ya Argentina ambapo alikuwa moja ya wachezaji muhimu walioisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Bashungwa ataja vipaumbele tisa Wizara ya Ulinzi
Wanawake 30 watekwa wakidaiwa kushindwa kulipa ushuru