Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kikosi chake kilikua na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi mnono, tofauti na sare ya mabao matatu kwa matatu waliyoambulia usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Newcastle Utd.

Van Gaal ambaye mwanzoni mwa juma hili alinukuliwa akisema, kuna wakati mwingine amekuwa hapendezwi na uchezaji wa timu yake lakini kwenye mchezo dhidi ya Newcastle Utd walicheza vyema na nusura waondoke na ushindi lakini Paul Dummett aliwanusuru The Magpies kwa kufunga bao la kusawazisha.

“Bila shaka ninahisi ni kama tulishindwa. Hatukutaka kushinda,” alisema Mholanzi huyo ambaye vijana wake walitangulia kwa kufunga mabao mawili kwa sifuri.

“Tungefunga mabao sita lakini lazima ufunge bao moja zaidi ya mpinzani wako.”

Katika mchezo huo kikosi cha Man Utd, kilifanya mashambulizi ya haja katika kipindi cha kwanza na mshambuliaji wao Wayne Rooney alifanikiwa kuandika bao la kwanza kwa penati kabla ya Jesse Lingard hajafunga bao la pili.

Newcastle United and Manchester United players join fans in a minute's silence in memory of former Magpies goalkeeper Pavel Srnicek

Baada ya Newcastle kusawazisha kupitia Georginio Wijnaldum na Aleksandar Mitrovic, Rooney alifunga bao la tatu huku Lingard na Marouane Fellaini walipoteza nafasi nzuri za kufunga kabla ya Dummett kusawazisha.

“Tulipoteza ushindi, nimewaambia hivyo wachezaji wangu,” Van Gaal ameongeza.

Katika hatua nyingine meneja huyo mwenye umri wa miaka 64, amekosoa maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya kikosi chake, kwa wenyeji kupewa penati baada ya Chris Smalling kudaiwa kumchezea vibaya Mitrovic, penati ambayo mshambuliaji huyo alifunga bao la kusawazisha.

“Refa alitoa penalti na hakukuwa na kosa lolote, ni wachezaji wawili walikuwa wanakabiliana, na huwezi kuamua ni nani amemfanyia mwingine madhambi.”

Joto La Usajili Wa Dirisha Dogo Laendelea Kupanda
Breaking News: Jerome Valcke Atimuliwa FIFA